Jumatano , 24th Feb , 2016

Watanzania wametakiwa kutokutumia vipodozi vyenye kemikali kali ambavyo husababisha madhara madhara mbalimbali ikiwemo magonjwa ya kansa na pamoja na ngozi.

Baadhi ya vipodozi vilivyopigwa marufuku na Mamalaka ya Chakula na Dawa (TFDA).

Idadi kubwa ya watumiaji wa vipodozi vyenye kemikali kali wengi wao ni wanawake ambao wamekuwa wahanga wakubwa wa tatizo hilo.

Muuzaji wa vipodozi ambaye ni mwenyeji wa nchi jirani ya Kenya, Shamimu Sambo amewataka kinamama kutumia vipodozi vya asili ambavyo havina madhara pamoja na kukubaliana na maumbile waliyonayo.

Muuzaji wa vipodozi nchini Tanzania, Hilda Makundi amesema kuwa Watanzania wanapaswa kuelimishwa juu ya matumizi ya vipodozi ili waweze kufanya uchaguzi sahihi utakaolinda afya ya ngozi zao

Japhet Naftal Mwanachama wa Kampuni ya vipodozi akizungumza Katika hafla ya utoaji tuzo kwa wauzaji bora wa vipodozi ambayo ilikutanisha wauzaji kutoka nchi za Afrika Mashariki amesema kuwa biashara ya vipodozi imekuwa ikitoa ajira kwa vijana wengi na kuwawezesha kujiajiri.