Jumatano , 26th Aug , 2015

Mkoa wa kigoma ni miongoni mwa mikoa saba nchini inayotekelza mradi wa kuboresha elimu ya msingi kwa kushirikiana na shirika la equip Tanzania baada ya kuwepo kwa wanafunzi waliomaliza darasa la saba huku wakiwa hawajui kusoma na kuandika.

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Luten Kanali Mstaafu Issa Machibya akiongea na Waribu wakatri wa kukabidhi Pikipiki

Kaimu afisa elimu wa mkoa wa Kigoma Venance Babukege amesema utekelezaji wa mpango wa kuwawezesha walimu wa darasa la kwanza na la pili katika shule 632 za msingi mkoani Kigoma unalenga kuwaendeleza walimu na kutoa vifaa lengo likiwa ni kuboresha taaluma hasa kwa wanafunzi wa shule za msingi.

Akikabidhi pikipiki kwa waratibu mkuu wa mkoa wa Kigoma Luten Kanal Mstaafu Issa Machibya amewataka waratibu kuzitumia kwa malengo yaliyokusudiwa na kwamba serikali haitasita kuchukua hatua kwa watakaokwenda kinyume.

Kwa upande wao waratibu wa elimu katika mikoa hiyo wamesema kuwa kazi ya ufuatiliaji na ukaguzi ilikuwa ngumu kutokana na tatizo la usafiri ambapo sasa kwa msaada huo itarahisisha kukuza sekta ya elimu mkoani humo.