Wanawake watakiwa kuchangamkia fursa za uongozi

Ijumaa , 16th Oct , 2020

Ushiriki wa Wanawake katika siasa na uongozi bado ni mdogo ukilinganishwa na wanaume nchini, kwani hadi sasa ni asilimia 37 pekee ya wanawake ndio wanaoshika nyadhfa za juu katika ngazi za maamuzi ikiwemo Bunge.

Mkurugenzi wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Rose Reuben.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Rose Reuben wakati akizungumza na wanahabari, viongozi wa dini pamoja na wazee wa kimila.

Bi. Rose amesema kuwa Wanawake bado wanakumbana na vikwazo katika ushiriki wao kisiasa, vikawazo vya kimila pamoja na sheria kandamizi zinambana mwanamke kushirki katika ngazi za uongozi.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika warsha hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo amesema kuwa katika kuhakikisha wanamkomboa mtoto wa kike Serikali inatoa vipaumbele vingi kwa Wanawake katika nafasi za uongozi.