Ijumaa , 3rd Jun , 2016

Baadhi ya Wabunge la Tanzania, wameonyesha wasiwasi juu ya watendaji wa Mahakama na makampuni ya uwakili dhidi ya kesi za mafisadi nchini na kusema hao ndio sababu ya serikali kushindwa kesi nyingi.

Mmoja kati ya Wabunge waliohudhuria semina ya Taasisi ya Kupambana na Kuzuia na Rushwa, Mbunge wa Nkasi (CCM), Ally Kessy.

Wabunge hao wameshangaa na kesi nyingi zinzowakabiliwa mafisadi wakubwa nchini zikiisha kwa wahusika kuonekana hawana hatia na kuifanya serikali kuingia hasara katika gharama za uendeshaji.

Wakiongea katika semina iliyotolewa na Taasisi ya Kuzia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) iliyofanyika Mkoani Dodoma Wabunge hao wamesema kuwa ufisadi mkubwa unaonekana bado unalelewa na wanasheria.

Aidha. Wabunge hao wamejinyooshea wenyewe vidole kwa kusema kuwa kuna baadhi ya wabunge, mawaziri pamoja na Jeshi la Polisi kwa kiasi wanahusika katika kuwalinda mafisadi hao ambao wanakabiliwa na kesi mbalimbali nchini.

Aidha, wabunge hao wamesema kuna haja ya kuwafundisha watoto maadili mema juu ya kupinga ufisadi ili taifa baadaye liweze kuwa na viongozi wenye uzalendo na wenye kuchukua rushwa.

Sauti ya Wabunge wanaolalamikia Wanasheria kukwamisha mapambano ya Ufisadi