Alhamisi , 19th Nov , 2020

Afisa Huduma za Uangalizi Wilaya ya Kinondoni Mwajabu Salum amesema si kweli kwamba wafungwa wengi wanaohukumiwa kifungo cha nje ni watu wa nyadhifa za juu bali walio wengi ni maskini.

Afisa Huduma za Uangalizi Wilaya ya Kinondoni Mwajabu Salum

Akizungumza katika kipindi cha Supa Breakfast, leo Asubuhi Mwajabu, amesema kuwa wafungwa wanao wasimamia ni wale ambao wanatoka moja kwa moja mahakamani au walifungwa mahakamani na adhabu zao azitakiwi kuzidi zaidi ya mikia mitatu.

“Tunaowafungwa zaidi ya mia sita na asilimia kubwa ya wafungwa wengi tulionao katika kifungo cha nje ni watu wakipato cha chini sio kweli waliowengi katika kifungo cha nje ni mabosi” amesema Mwajabu Salum

Aidha Mwajuma amesema kuwa Kifungo cha nje ni adhabu mbadala kwa ajili ya kudhibiti msongamano wa wafungwa gerezani ambayo husaidia kuihusisha jamii kufanya urekebishaji wa jamii huku akiongeza kuwa adhabu hii humuwezesha mfungwa kuendelea na shughuli zake nyingine za kujiingizia kipato.