Mwishoni mwa mwaka jana wanafunzi walikosa sifa ya kupewa mikopo ya elimu ya juu, waligubikwa na majonzi na vilio huku wengine wakipiga kambi katika ofisi za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu jijini Dar es salaam, kuomba kupatiwa mikopo wakihofiwa kushindwa kuendelea na masomo yao licha ya kuwa wamechaguliwa kuendelea na masomo ya elimu ya juu katika vyuo mbalimbali.
Veneranda Malima ambaye ni Afisa Uhusiano wa bodi hiyo amesema baada ya kupitia rufani jumla ya wanafunzi 2,000 watapewa mikopo ambapo amewaondoa hofu wanafunzi waliokosa mikopo na kuwataka kuambatanisha nyaraka na viambatanisho vyote muhimu kama inavyotakiwa kwani lengo la bodi hiyo ni kuona wanafunzi wote wenye sifa wanapewa mikopo na kuendelea na masomo yao.