Wanafunzi wakiwa darasani.
Waziri Jafo ametoa kauli hiyo leo Desemba 5, 2019, Jijini Dodoma, wakati akitangaza idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Sekondari kwa mwaka 2020, na kuagiza viongozi wa Mikoa kuhakikisha wanamaliza ujenzi wa vyumba vya madarasa na vyoo kabla ya Februari 29, 2020 ili yaanze kutumika March 2, mwaka huo.
Aidha Waziri Jafo amesema kuwa jumla ya Wanafunzi 701,038, sawa na asilimia 92.14 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha Kwanza kwa mwaka 2020 kati ya wanafunzi 760,803 waliofaulu Mtihani wa kumalizia Elimu ya Msingi.
Waziri Jafo ameongeza kuwa Mikoa 13 ya Geita, Morogoro, Dodoma, Njombe, Katavi,Singida,Ruvuma,Tabora,Kilimanjaro, Kagera, Mwanza, Shinyanga na Mtwara wanafunzi wote wamefaulu kwenda katika Shule za Serikali.