Wamiliki wa malori kuwajibishwa

Jumamosi , 2nd Jan , 2021

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Tanzania, Wilbroad Mutafungwa, ametoa maagizo kwa wamiliki wa magari makubwa kuhakikisha wanatoa stahiki kwa madereva na kutoa mikataba sahihi ili kupunguza ajali za barabarani nchini.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Tanzania, Wilbroad Mutafungwa

Akiwa katika ziara yake mkoani Songwe, Kamanda Mutafungwa alikutana na madereva wa malori na It na kuwasisitizia madereva hao matumizi sahihi ya sheria na alama za barabarani.

"Wako baadhi ya wamiliki wa makampuni ambao wao ukimuambia gari haina tairi anakuambia lete dereva mwingine tuendelee na safari, wamiliki wa aina hiyo hakika wanakuwa wameshiriki kwa kiasi kikubwa kuangamiza watu tutakapogundua gari limebeba mzigo ni bovu tutamwajibisha dereva na tutatafuta jinsi ya kumwajibisha mmiliki", ameongeza Kamanda Mutafungwa.