Jumatatu , 5th Oct , 2015

Wahitimu wa bodi ya ya taifa na wakaguzi wa Hesabu nchini Tanzania (NBAA) ambao ni wataalamu wa masuala ya uhasibu na ukaguzi wa hesabu wameaswa kulinda na kusimamia viapo vyao wakati wakitekeleza majukumu yao ya kihasibu.

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais( Kazi maalumu) Prof. Mark Mwandosya.

Akizungumza katika mahafali ya ya Bodi hiyo Waziri wa nchi Ofisi ya Rais( Kazi maalumu) Prof. Mark Mwandosya amesema kiapo chao kiwe chachu ya ufanisi katika utendaji wa kazi kwani kushuka kwa kiwango cha maadili katika utumishi wa Umma kunatokana na Suala la Fedha.

Aidha Prof. Mwandosya ameongeza kuwa bodi ya NBAA na watanzania wana wajibu wa kujenga fikra ya kizalendo kwa taifa lao na kujiamini katika masuala ya hesabu za fedha ili wafikie viwango vya kimataifa kwa kuweka misingi imara.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa NBAA, Pius Maneno amesema kituo hicho kinatoa mchango mkubwa nchini katika kukuza fani ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu tofauti.