Alhamisi , 31st Mar , 2016

Wabunge watatu ambao ni wajumbe wa zamani wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali za Mitaa LAAC, leo wamefikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na tuhuma za kudai rushwa.

Wabunge watatu ambao ni wa wajumbe wa zamani wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali za Mitaa, leo wamefikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na tuhuma za kudai rushwa.

Wabunge hao waliofikishwa mahakamani hapo na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ni Mbunge wa Mwibara Alphaxad Kangi Lugola, Suleiman Ahmed Sadick na Mbunge wa Lupa Victor Kilasile Mwambarasa

Wakisomewa shitaka lao Mbele ya Hakimu Thomas Simba imedawa kuwa wabunge hao walishawishi kupewa rushwa ya shilingi milioni 30 kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Gairo, Mbwana Magota, kwa lengo la kutoa mapendekezo mazuri ya hesabu za serikali yake.

Washtakiwa hao wote watatu wamekana shitaka hilo na wameachiwa huru kwa dhamana ya shilingi milioni 5 kila moja na mdhamini moja kila mmoja ambapo kesi hiyo itatajwa tena tarehe 14 mwezi wa Nne mwaka huu.