Ijumaa , 16th Oct , 2015

Baraza la habari Tanzania (MCT), limewahimiza waandishi wa habari nchini kuweka pembeni hulka zao za kisiasa na kuzingatia ueledi na maadili ya uandishi wa habari hasa kipindi hiki cha uchaguzi.

Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga

Rai hiyo imetolewa leo jijin Dar es salaam na Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga wakati akizinduwa mashindano ya tuzo za umahiri wa uandishi ambazo zitafanyika mwezi April 2016.

Mukajanga ameongeza kuwa katika kipindi hiki cha kampeni, taifa linawategemea sana waandishi wa habari na hivyo wasitoe taarifa na habari kwa kuegemea upande wa chama anachokipenda bali wafuate misingi ya habari na uweledi pamoja na kuandika habari za kuchochea amani na utaifa zaidi.

Aidha Mukajanga amewataka waandishi wa habari kuandika habari za kodi ili kuchochea watu wapende kulipa kodi pamoja na habari juu ya manunuzi ya umma ili kudhibiti manunuzi yasiyofuata sheria na kupelekea taifa kupata hasara.