Jumatatu , 20th Jul , 2015

Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, imesema kutakua na vituo 1669 vya kuandikisha wapiga kura kwa mfumo wa BVR, jijini Dar es Salaam Zoezi linalotarajiwa kuanza hapo keshokutwa.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Tanzania Jaji Mstaafu Damian Lubuva.

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Mstaafu Damian Lubuva na kuongeza kuwa kila kituo kitakuwa na BVR kits mbili na zitaendelea kuongezwa kwa kadri ongezeko la watu wanaostahili kuandikishwa kwenye kituo husika.

Aidha Jaji Lubuva amewataka wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kjwa tika Daftari hilo kwa mujibu wa sheria ili aweze kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba.

Ameongeza kuwa vituo vitafunguliwa kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa 12 na mbili jioni huku akisema kuwa kituo kitatoa kipaumbele kwa wanawake wajawazito, wazee na wenye ulemavu wa aina mbalimbali.