Jumanne , 2nd Aug , 2016

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amewataka vijana kuendana na kauli mbiu ya Serikali ya hapa Kazi tu ili iweze kuleta tija kutokana na Uchumi wa nchi kutegemea zaidi mchango wa vijana katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Waziri Mkuu Majaliwa amesema hayo jana wakati akifungua Maonesho ya 24 ya wakulima maarufu kama nane nane kwa kanda ya Mashariki yaliyofanyika mkoani Morogoro katika viwanja vya mwalimu Julias Kambarage nyerere.

Mhe. Majaliwa amesema kuwa uchumi wa nchi unategemea zaidi kilimo hivyo amewataka vijana kujitokeza kwa wingi ili kuweza kufanya kilimo chenye tija kwao na taifa kwa ujumla na kufikia malengo yaliyowekwa na serikali.

Aidha Waziri Mkuu amesema kuwa kutokana na mkoa huo na matukio mengi ya migogoro ya wakulima na wafugaji serikali imeweka suluhisho ambalo litakua la kudumu ikiwemo kugawa vitalu kwa wakulima na wafigaji.

Sauti ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,