Ijumaa , 16th Oct , 2020

Zikiwa zimesalia siku 11 kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Octoba 28,2020 baadhi ya Vijana kutoka Vyuo vikuu hapa nchini kwa kushirikiana na baadhi ya vijana wenye vipaji mbalimbali na wengine wa kada tofauti wamepanga kufanya matembezi ya amani katika viwanja vya Tanganyika packers, jumamosi hii.

Jumuiya ya vijana wenye ulemavu wakiwa katika picha ya pamoja na vijana kutoka kada na tasnia mbalimbali.

Katika viwanja hivyo tarehe 17, makundi yote yamelenga kukumbusha ulinzi wa amani na kwamba vijana ndio wenye jukumu kubwa la kuamua mustakabali wa Taifa lao hivyo pasi na shaka jukwaa hilo litawaleta pamoja licha ya tofauti zao za vyama, itikadi wakiunganishwa wote na utanzania.

Kwa upande kundi la vijana ambao hujishugulisha na ujasiriamali, uimbaji, usanii katika kuchora, kuigiza wote wakikusanyika kwa pamoja ili kuhakikisha vijana wanaachwa kutajwa katika kundi la watu ambao wanahofiwa kuingizwa katika vurugu.

Kwa mujibu wa ratiba kutoka Tume ya Taifa ya uchaguzi zimebakia takribani siku 11 tuu kwa Wananchi kujitokeza kushiriki katika zoezi la uchaguzi Mkuu wa October 28 na kwamba ulinzi wa amani ndiyo tunu ya Taifa la Tanzania