Jumamosi , 5th Mar , 2022

Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo,amewasamehe Vijana 854 wa JKT waliofukuzwa makambini April 12,2021 kutokana na utovu wa nidhamu.

Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo

Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano (JWTZ)Luteni Kanali Gaudentius Gervas Ilonda, amesema kati ya vijana 854, mmoja amefariki na wengine 853 wapo hai na wanatakiwa kuripoti kambini.

"Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linapenda kutoa taarifa kwa Umma wa Watanzania kwamba Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo ametoa msamaha kwa Vijana wote 853 na ametoa maelekezo na ameamuru Vijana hao wote warejeshwe katika Makambi ya Kujenga Taifa tayari kwa kuanza mafunzo yao mara moja", ameeleza Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano (JWTZ) Luteni Kanali Gaudentius Gervas Ilonda.