Jumapili , 10th Jan , 2021

Klabu ya Simba SC imethibitisha nyota wake Clatous Chama kuwa amesaini mkataba mpya wa kuendelea kukipiga msimbazi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba C Mohammed Dewji (kushoto), Clatous Chama (katikati) na Barbara Gonzalez (kulia).

Simba SC kupitia kwa Afisa Habari wake Haji Manara, imetoa picha huku akieleza kuwa sasa mwisho wa uzushi ambao ulikuwa unasambaa kuwa hajasaini mkataba.

Licha ya Simba SC kutoweka wazi juu ya urefu wa mkataba ambao Chama amesaini lakini vyanzo vya ndani vimeeleza kuwa amesaini mkataba wa miaka mitatu.

Suala la Chama kuongeza mkataba limekuja siku moja tu baada ya timu hiyo kuachana na aliyekuwa kocha wao mkuu Sven Vandenbroeck ambaye ametimkia klabu ya FAR Rabat ya Morocco ambako amesaini mkataba wa  miaka miwili.