Jumamosi , 23rd Mar , 2024

Wananchi zaidi ya 2,400 kutoka kijiji cha GIDABAGHARA wilaya ya Babati mkoani Manyara wanaounda kaya takribani 500 wamesema kukosekana kwa huduma ya maji safi na salama kijiji hapo kumeleta athari hasi kama vile kudhorota kwa amani, kuvunjika kwa ndoa na wengine kupata ujauzito.

Chanzo cha Maji ya Kisima

Wakizungumza na EATV baadhi ya wananchi wameleza kuwa changamoto hiyo ambayo imedumu kwa miaka kadhaa sasa inakwenda kuondoka na wao kunusuru ndoa zao, kuondokana na athari za vifo vilivyotokana na maradhi ya mlipuko baada ya kutumia maji ya visima ambayo si safi na salama. 

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga wakati akifungua mradi wa maji wenye gharama ya zaidi ya TZS. milioni 290 uliowezeshwa na shirika la World Vission ameielekeza mamlaka ya RUWASA mkoani humo kuhakikisha zoezi la usambazaji wa maji kupitia mradi huo linakuwa na gharama nafuu kwa wananchi.

Kwa upande wake Meneja wa Shirika la World Vission Kanda ya Kaskazini anaeleza kuwa mradi huo umesaidia kupunguza mwendo wa zaidi ya saa moja kwa wananchi kuyafuata maji na sasa wakiyapata maji hayo kwa dakika tano mpaka kumi.