Jumanne , 17th Jan , 2017

Serikali ya Uganda imetangaza mlipuko wa mafua ya ndege aina ya H7N9, ambapo mizoga kadhaa ya ndege imekutwa katika wilaya za katikati mwa nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Waziri wa Kilimo, Viwanda na Uvuvi nchini Uganda, Christopher Kibazanga.

Kulingana na Waziri wa Kilimo, Viwanda na Uvuvi, Christopher Kibazanga, vipimo vilivyofanywa nchini humo vimethibitisha mlipuko wa mafua ya ndege yenye virusi vinavyosambaa upesi na kusababisha vifo vingi zaidi kwa binadamu na wanyama.

Kibazanga amesema mnamo tarehe pili mwezi huu wa Januari, mamlaka wa wanyamapori waliripoti vifo vingi vya ndege.

Wizara hiyo bado haijatoa takwimu kamili za ndege walioathirika na wala kiwango cha mambukizo ya virusi hivyo vya H7N9.