Jumanne , 7th Jun , 2016

Abiria wanautumia usafiri wa Mabasi ya mwendo wa Haraka jijini Dar es Salaam wameomba serikali kuharakisha kufanya mchakato wa kukata tiketi kwa kutumia kadi za kielektroniki ili kuondokana na usumbufu

Abiria wakiwa ndani ya Basi yaendayo Haraka

Abiria wanautumia usafiri wa Mabasi ya mwendo wa Haraka jijini Dar es Salaam wameomba serikali kuharakisha kufanya mchakato wa kukata tiketi kwa kutumia kadi za kielektroniki ili kuondokana na usumbufu ikiwa ni pamoja na misururu mirefu inayosababishwa na hali hiyo katika vituo vya kukatia tiketi.

Usafiri huo unaoanzia Kimara mwisho na kupitia Ubungo kuelekea Kariakoo pamoja na Kivukoni, Mabasi yenye uwezo wa kubeba abiria 150 kwa mabasi makubwa na 90 kwa mabasi ya uwezo wa kati, abiria wengi wamekuwa wakichangamkia kutumia usafiri huo kutokana na ufanisi wake japo si kwa kiwango kikubwa kama ilivyotarajiwa.

Mapema asubuhi katika vituo vya kupandia usafiri huo kumekuwa na misururu mirefu ya wasafiri wakikata tiketi ili kuwahi katika pilikapilika za siku, huku wengi wao wakisema hali hiyo imechangiwa na matumizi ya tiketi badala ya kadi na kufanya zoezi hilo kwenda taratibu na kusababisha usumbufu mkubwa

Akizungumzia kasoro hizo Msimamizi wa kituo Cha kivukoni Nelson Christopher Mwaisango anasema wanaendelea kushughulikia dosari lizizojitokeza katika mashine za kukatia tiketi ili siku zijazo usafiri huo uwe na ufanisi zaidi huku matumizi ya kadi yakiendelea kufanyiwa mchakato wake

Benedict Mapunda ni Dereva wa basi linalosafirisha abiria kati ya Kimara na Kivukoni anasema bado wananchi hawana uelewa wa matumizi ya mabasi hayo