Alhamisi , 28th Apr , 2016

Wakati mradi wa Mabasi yaendayo kasi ukiwa katika majaribio imebainika kuwa miundombinu ya mradi huo imeanza kuharibiwa na watu wasiojulikana ikiwemo uharibifu wa magari hayo yanayotarajiwa kutumika.

Msemaji wa UDA-RT,Sabri Mabrouk, akizungumza na wanahabari hawapo pichani

Akizungumza na East Africa Radio, Msemaji wa UDA-RT,Sabri Mabrouk,amesema kuwa mpaka sasa ajali 21 zilizotokana na watu kuvamia miundombinu ya barabara hizo zilizotengwa maalumu kwa ajili ya mradi huo.

Bw. Mabrouk amezitaka taasisi husika ikiwemo jeshi la polisi usalama barabara waongeze adhabu kwa mtu atakayebainika kuharibu miundombinu hiyo kwa makusudi ili kukomesha uharibufu huo unaofanywa na baadhi ya watu wasiojulikana.

Aidha Mabarouk ameviomba vyombo vya habari na wana usalama barabarani kuendelea kutoa elimu juu ya utunzanji wa miundombuni hiyo pamoja na magari yake ili mradi huo udumu kwa muda mrefu na kuwasaidiwa wakazi wa Dar es Salaam, katika kurahisisha usafiri na kuwaondolea adha ya foleni.

Sauti ya Msemaji wa UDA-RT,Sabri Mabrouk