Jumatatu , 15th Dec , 2014

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji uliofanyika jana nchini Tanzania ulitawaliwa na kasoro na vurugu zilizosababisha polisi kutumia risasi na mabomu ya machozi huku baadhi ya wapiga kura wakipigana sehemu tofauti tofauti nchini.

Mkurugenzi wa Serikali za Mitaa bw. Khalist Luanda

Vurugu hizo zilitokana na uchaguzi huo kugubikwa na kasoro nyingi na hivyo kusababisha baadhi ya vituo kulazimika kuahirisha uchaguzi hadi wiki ijayo.

Vurugu hizo ziliripotiwa katika mkoa wa Dar es Salaam, Morogoro, Mwanza, Kigoma, huku kasoro hizo zikitajwa kuwa baadhi ya vituo kuchanganya majina ya wagombea, kuchelewa kuanza kwa uchaguzi, kukosekana kwa vifaa vya kupigia kura na Mengineyo.

Katika vurugu zilizojitokeza Jijini Dar es Salaam Jeshi la Polisi Wilaya ya Kinondoni linawashikiliwa watu watatu kwa mahijiano zaidi kama anavyoelezeka kamanda Kamanda Camillus Wambura.

Wakati Sehemu nyingine zikitawaliwa na vurugu hizo na hatimaye kura kupigwa lakini kuna baadhi ya mikoa ikiwemo Kigoma na Ruvuma wananchi wa baadhi ya sehemu walishindwa kabisa kupiga kura kutokana na kutokukamilika kwa taratibu zingine.

Licha ya sehemu hizo imeripotiwa kuwa mamia ya wananchi wa maeneo mbalimbali mkoani Arusha wamejitokeza kupiga kura kwa amani na utulivu hali iliyoashiria baadhi ya wananchi kuanza kupata uelewa na masuala ya kisiasa na kutambua haki zao.

Na katika matokeo ya awali kwa baadhi ya mikoa imeonesha kuwa sehemu kubwa ya uongozi umeangukia mikononi mwa vyama vya upinzani.