Alhamisi , 23rd Jun , 2016

Serikali ya Tanzania imeitaka jamii kutowabagua vijana walioathirka na madawa ya Kulevya, na badala yake ijikite katika kupambana na wasambazaji wa madawa ya kulevya nchini ikiwemo kuwafichua kutoka maeneo wanayoishi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe, Jenista Muhagama.

Hayo yamesema na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe, Jenista Muhagama, wakati wa ziara ya kukagua kituo cha huduma kwa vijana waliothirika na dawa za kulevya kinachojengwa eneo la Itega nje kidogo ya mji Dodoma.

Mhe. Mhagama amesema kuwa vijana wengi kwa sasa wanajikuta wakiingia katika matumizi ya dawa za Kulevya bila kujijua kutokana na mbinu zinazofanywa siku hizi ikiwemo kuweka dawa hizo katika uvutaji wa Shisha.

Waziri Muhagama amesema licha ya Serikali kuendelea kuhudumia matibabu kwa waathirika wa dawa za kulevya, itaendelea kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya kwa kuwa inamaliza nguvu kazi ya taifa ambayo wengi wao ni vijana.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Hospitali ya Mirembe Dkt. Erastus Mdeme, amesema kuwa licha ya ujenzi wa kituo hicho kukamilika lakini wanakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo upungufu wa wahudumu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe, Jenista Muhagama,