Jumatatu , 1st Aug , 2016

Chama cha Wafanyakazi ngazi ya serikali za mitaa (TUGHE) kimewataka waajiri kuondoa tatizo la mikataba iliyopitwa na wakati ambayo haiendani na mazingira halisi na badala yake waiboreshe ili iweze kutoa haki za msingi za wafanyakazi

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mrisho Gambo

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi mkoa wa Arusha (TUGHE) Ndugu Pascal Sighis katika mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa TUGHE kwa ngazi ya mkoa ambapo amesema kuwa tatizo la mikataba iliyopitwa na wakati imekithiri katika sekta nyingi hususan sekta za afya hivyo amesema kuwa kazi watakayoanza nayo ni kupita kwa waajiri na kukagua mikataba iwapo inaendana na wakati uliopo.

Amesema kuwa wako baadhi ya Waajiri ambao wamekua wakiwalazimisha wafanyakazi kusaini mikataba hiyo na kuwatishia kuwafukuza kazi iwapo hawatasaini jambo ambalo linakiuka haki za wafanyakazi.

Katibu wa TUGHE Magero Samweli na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mrisho Gambo wamesema kuwa Viongozi wa Mkoa waliochaguliwa wanajukumu la kutetea haki za wafanyakazi na stahiki zao bila woga.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mrisho Gambo na Afisa Kazi mkoa wa Arusha Yusuph Nzugile amesema kuwa Maofisa wa kazi wamejipanga kuanza ziara ya kuwatembelea waajiri na kutazama mikataba iwapo inakiuka sheria za kazi ama inaendana na sheria ili waweze kujiridhisha na kuwachukulia hatua za kisheria.