Jumatatu , 20th Jul , 2015

Baada ya kutunga sheria mpya ya Ongezeko la Thamani VAT, ya 2014 Mmamlaka ya Mapato Tanzania TRA, imeanza kutekeleza sheria hiyo huku ikiwataka walipa kodi kuisoma na kuifuata bila shuruti.

Rished Bade kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Afisa kodi mwanadamizi wa TRA, Donasian Assey amesema serikali imefanya mabadiliko ya sheria kutokana na iliyyokuwepo kuwa na upungufu mkubwa na kuikosesha serikali mapato.

Assey amesema sheria mpya imefafanua jinsi ya ulipaji kodi na watu wanaotakiwa kulipa wakati mwaka 1997 ilikuwa haielezi na kuainisha maenep ya kusamehewa kodi.

Naye Afisa TRA Bw. Peter Kiatu amesema kutokana na sheria iliyofutwa kuwa na upungufu serikali ilitenga kukusanya kodi asilimia sita ya pato la taifa kwa mwaka badala yake ilikusanya asilimia 4.8 hivyo ilikuwa ikipoteza mapato na kupata hasara.