Ijumaa , 8th Jan , 2016

Mamalaka ya mapato Tanzania imetakiwa kufungua ofisi yake mkoa wa Njombe ili kurahisisha huduma kwa jamii na kuepusha usumbufu wa kuzifuata huduma hizo mikoa ya Iringa, Mbeya na Ruvuma.

Mkuu wa mkoa wa Njombe Dr. Rehema Nchimbi.

Ombi hilo limetolewa na baadhi ya wafanya biashara na madereva mkoani Njombe kwa nyakati tofauti wakati wakizungumzia kauli ya mkuu wa mkoa wa Njombe Dr. Rehema Nchimbi kuwa mkoa huo sio mpya na taasisi za serikali zinatakiwa kuhamishia ofisi za kimkoa mkoani humo.

Mmoja wa wafanyabiashara bw, Ezekiel Tweve mfanyabiashara ndogondogo mkoani Njombe anasema kuwa wamekuwa wakipata shida kupata TIN Namba ambazo wanahitajika kufuata mpaka mkoani Iringa ambako ndiko inadaiwa kuwa ni ofisi za TRA mkoa wa Njombe na Iringa.

Mkuu wa mkoa wa Njombe Dr Nchimbi ametoa agizo kwa ofisi za umma kufungua ofisi za kimkoa mkoani humo kwa kuwa mkoa huo sio mpya tena.