Jumatatu , 15th Feb , 2016

Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Mkoa wa Shinyanga imeufunga mgodi wa El-Hilal Minerials Limited unaochimba Almasi Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga, baada ya kushindwa kulipa kodi ya mapato kiasi cha sh. Milioni 374.

Meneja wa TRA mkoa wa Shinyanga bwana Ernest Dundee

Meneja wa TRA, mkoa wa Shinyanga, Ernest Dundee amesema hatua hiyo ilisababisha ofisi yake kumtumia kwa kumpa mamlaka dalali ambaye ni wakala wake wa kukusanya mapato kwa wadaiwa sugu, Kampuni ya Suka Security Co.Ltd kufuatilia deni hilo.

Meneja huyo ameongeza kuwa zoezi hilo litakua endelevu na kutoa wito kwa wafanyabishara na wananchi kwa ujumla kulipa kodi ya mapato kwa wakati bila shuruti ili kuepukana na usumbufu unaoweza kujitokeza baadaye.

Akizungumzia kazi hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Suka Security co, Lyasuka Ibrahimu amesema kwa mamlaka aliyopewa alifika mgodini hapo kukusanya mapato kwa wateja wake ambao walikaidi kulipa kodi ya mapato halali ya serikali.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa kwa mujibu wa sheria ya TRA, kumpa dalali huyo kwenda kukumbushia kulipwa mapato hayo kulishindikana baada ya kaimu meneja uzalishaji wa mgodi huo, Badul Seif kukataa kusaini barua ya kufunga vinu vya kusaga mchanga na kusafisha Almasi.