Ijumaa , 13th Jun , 2014

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania TMA imewataka watanzania kuzingatia utabiri wa hali ya hewa ili kuepukana na madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na hali ya hewa itakavyotabiriwa.

Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya hali ya hewa Tanzania TMA Dkt Agnes Kijazi.

Hata hivyo kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania tathmini inaonyesha kuwa muamko wa wananchi kuendesha maisha yao kwa kufuatilia utabiri wa hali ya hewa sio wa kuridhisha japo umeongezeka kwa kiasi kidogo.

Akizungumza na East Africa Radio katika ofisi za Mamlaka ya Hali ya Hewa Meneja Huduma Utabiri Bw. Samuel Mbuya amesema kwa sasa wananchi wengi hususan wakulima wanaonekana kuanza kufuata utabiri wa hali ya hewa katika shughuli zao za kilimo.