Jumamosi , 31st Oct , 2015

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania TMA imewataka wananchi kujihadhari na mvua za El-Nino zilizoanza kunyesha katika baadhi ya mikoa hapa nchini.

Dkt. Ladislaus Chang'a

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania TMA imewataka wananchi kujihadhari na mvua za E-lnino zilizoanza kunyesha katika baadhi ya mikoa hapa nchini.

Tahadhari hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Ladislaus Chang'a wakati akiongea na East Africa Radio na kuongeza kuwa mifumo ya hali ya hewa inaonesha kuimarika kwa dalili ya kuwepo kwa mvua nyingi.

Dr Chang'a ameongeza kuwa kwa sasa dunia inakabiliwa na changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa inayosababisha joto kuongezeka, mvua kubwa, ukame na upungufu wa chakula.

Wakati huo huo Dr. Chang'a amesema mikoa ya Magharibi, kanda ya ziwa na Pwani ya kaskazini imeshaanza kupata mvua, hivyo wananchi wa mikoa hiyo wachukue tahadhari kubwa ikiwa ni pamoja na kutengeneza mifereji ili maji yasikusanyike eneo moja na kusababisha mafuriko.