Jumanne , 2nd Dec , 2014

Watu tisa wanadaiwa kuuawa katika mapigano baina ya jamii ya wafugaji w kabila la Wabarbaig maarufu kama Wamang'ati na wasukuma wilayani Kisarawe Mkoani Pwani nchini Tanzania.

Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani Ulrich Matei.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa polisi mkoa huo Ulrich Matei amesema chanzo cha mgogoro ni baada ya mfugaji jamii ya Wamang'ati kutuhumiwa kuiba Ng'ombe zaidi ya watano wa mfugaji wa kisukuma.

Kamanda amesema baada ya wizi huo vijana wa Kisukuma walianza msako na walimpomkamata mtuhumiwa walishambulia hadi kumuua na ndipo wafugaji wa Kimang'ati walipoamua kulipiza kisasi.

Aidha Kamanda Matei amesema Uchunguzi zaidi unaendelea ili kubaini majina ya watu waliouawa na kuwasaka watuhumiwa wa mauaji hayo.