Jumatatu , 4th Jan , 2016

Mamlaka ya dawa na chakula kanda ya kaskazini imeteketeza vipodozi vilivyopigwa marufuku kuingia nchini vyenye thamani ya shilingi milioni 34 na laki tisa baada ya kuvikamata katika mpaka wa Namanga mkaoni Arusha.

Vipodozi vyenye viambata vya sumu vikiteketezwa na Mamlaka ya dawa na Chakula (TFDA).

Meneja wa TFDA kanda ya kaskazini Bw. Damas Matiko amesema kuwa mapema mwaka jana maafisa wa mamlaka hiyo wakishrikiana na maafisa wa mamlaka ya mapato nchini TRA walikamata gari la kampuni ya parfect trans ikiwa na shehena hizo za dawa.

Aidha Bw. Matiko ameongeza kuwa bidhaa hizo zilikua na viambata vya sumu ambazo huleta madhara kwa watumiaji a mara nyingine hata vizazi vijavyo.

Hata hivyo uingizwaji wa bidhaa hizo umeanishwa na ukwepaji wa kodi ambapo kaimu afisa forodha wa mpaka wa Namanga Aminieli Malisa amesema kuwa amesema wamejiimarisha katika kusimamia uingizwaji wa biadhaa hizo.