Ijumaa , 20th Nov , 2020

Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Jestus Nyamanga, amekanusha taarifa za kuwa Bunge la Umoja wa Ulaya limeazimia kuifutia Tanzania msaada wa Euro Milioni 626 kitu ambacho siyo ukweli na kusema kuwa hakuna majadiliano yoyote yanayoendelea kwa ajili ya kuiwekea Tanzania vikwazo.

Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Jestus Nyamanga.

Kauli hiyo ameitoa mara baada ya taarifa kusambaa mitandaoni kwamba Bunge hilo limeazimia kuiwekea vikwazo hivyo Tanzania jambo ambalo halina ukweli wowote, ambapo ameongeza kuwa uhusiano kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya ni mzuri sana.

"Kikao kilichofanyika leo ni kikao cha kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na siyo cha Bunge lote la Umoja wa Ulaya na hata kikao hicho hakikutoa azimio lolote kuhusu Tanzania, na ni wabunge watano tu walitoa mawazo yao kati ya wabunge 71 wa kamati hiyo ya Mambo ya Nje, taarifa zinazoenezwa siyo za kweli na zinafanywa na watu wenye nia mbaya na Tanzania", amesema Balozi Jestus Nyamanga.