Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.
Mhe. Majaliwa ametoa kauli hiyo leo mchana wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika nyumbani kwake Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Akitoa ufafanuzi wa sukari ambayo imekwishawasili nchini, Waziri Mkuu alisema tani 2,000 zitapelekwa mikoa ya Kaskazini, tani 3,000 (mikoa ya Kanda ya Ziwa), tani 2,000 (mikoa ya Kusini), tani 2,000 (Nyanda za Juu Kusini) na tani 2,000 (mikoa ya Kanda ya Kati).
Amesema tani nyingine 24,000 za sukari zitawasili Ijumaa hii na hadi zitoke bandarini itakuwa kama Jumapili kwa hiyo zinaweza kusambazwa kuanzia Jumatatu. Tani nyingine 20,000 zitawasili baadaye, ama mwishoni mwa mwezi huu au mapema mwezi Juni.
Amewataka wasambazaji wa sukari waziuze kwa wafanyabishara wadogo ili wao wawawuzie wananchi kwa bei elekezi ya sh. 1,800. Pia amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanasimamia zoezi la ukaguzi ili kubaini zaidi wale waliohodhi bidhaa hiyo.