Jumanne , 14th Nov , 2017

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imesema kuwa agizo la kuhusu kumchunguza aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu imelisikia na imeanza kulifanyia kazi.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Mkurugenzi wa Takukuru, Brigedia Jenerali,  John Mbugo ameitoa leo akizungumza na wanahabari ikiwa ni siku moja baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangala kumtuhumu Nyalandu  kwa matumizi mabaya ya madaraka.

Brigedia Jenerali,  John Mbungo amesema kuwa endapo wakimkuta Nyalandu na hatia watamfikisha panapostahili.

Dk Kigwangalla  jana bungeni wakati akichangia Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 207/2018 aliiagiza Takukuru na polisi kumchunguza Nyalandu kwa madai kwamba aliisababishia serikali kukosa mapato na tuhuma zingine zenye kuhusisha rushwa. 

Dk Kigwangala alisema Nyalandu aliikosesha Serikali mapato ya Sh32 bilioni kwa miaka miwili aliyohudumu katika wizara hiyo kwa kushindwa kusaini sheria ya tozo kwa hoteli za kitalii.

Hata hivyo Mh. Nyalandu kupitia mitandao ya kijamiii amekuwa akikanusha tuhuma alizoelekezewa na Waziri Kigwangala na kusema kuwa hizo ni tuhuma zenye lengo la kumchafua pamoja kuwaogopesha watu wengine wenye nia ya kuhama Chama Cha  Mapinduzi.