Jumatatu , 9th Jun , 2014

Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) imewataka watumiaji wa vyombo vya baharini kuchukua tahadhari dhidi ya pepo za kusini ambazo huvuma katika bahari ya Hindi kati ya Juni na Agosti.

Picha ya ajali ya kuzama kwa meli ya MV Skagit, ajali iliyotokea jirani na kisiwa cha Chumbe Zanzibar Julai 18 mwaka juzi.

Tahadhari hiyo ilitolewa na mkurugenzi wa huduma za utabiri wa TMA, Hamza Kabelwa akisistiza kuwa wananchi hawana budi kuchukua tahadhari pindi taarifa zinapotolewa.

Aliendelea kusema kuwa Elimu juu ya masuala ya utabiri inapaswa kuwa endelevu kutokana na madhara makubwa ambayo yamekuwa yakitokea yakiwamo mafuriko yaliyotokea hivi karibuni kutokana na mvua za masika katika maeneo mengi nchini.