Jumapili , 6th Dec , 2015

Baadhi ya vyumba vya madarasa kikiwemo chumba cha kuhifadhia vitabu katika shule ya msingi Daraja mbili iliyoko jijini Arusha vimeteketea kwa moto ambao bado chanzo chake hakijajulikana.

Baadhi ya Majengo ya Shule ya Msingi Daraja mbili yaliyotketea kwa moto

Pia moto huo umeteketeza kadi za taarifa za maendeleo ya wanafunzi, ikiwa ni masaa machache kwa moto huo kutokea mara baada ya kufungwa kwa shule hiyo kwa likizo ya mwisho wa mwaka.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Steven Kweka amesema kwa sasa bado hawajafanya tathmini kujua thamani ya vitu vilivyoteketea ila anaomba jitihada za haraka zifanyike kuzuia athari zinazoweza kutokea kutokana na tukio hilo.

Mkuu wa wilaya ya Arusha Fadhili Nkurlu ametembelea etembelea shuleni hapo amesema tayari amewaagiza waandisi kufanya tathmini ya vyumba vilivyoungua kwa lengo la kuanza ukarabati, pia ametoa wito kwa wananchi na taasisi kujitokeza kuchangia shule hiyo