Alhamisi , 23rd Oct , 2014

Shirikisho  la  watu  wenye  ulemavu  nchini  SHIVYAWATA limeipinga Katiba Inayopendekezwa kwa madai kuwa imeacha mambo mengi muhimu kwa walemavu.

Shirikisho  la  watu  wenye  ulemavu  nchini  SHIVYAWATA  limeibuka  na kusema  kuwa  katiba inayopendekezwa  kwa  ajili  ya kupigiwa kura  na wananchi  haipo  kwa  maslahi  ya  taifa  bali inalinda  watu   wachache wenye  nguvu  na  kuacha  mambo  mengi ambayo  yalipendekezwa na shirikisho  hilo.
 
Kauli  hiyo  imetolewa  mjini  Musoma  na  mjumbe   wa  bodi   ya  shirikisho hilo   nchini  Bw Batista Mgumu, wakati  akizungumza kwenye  mkutano wa  kujadili  wa  haki   na  usawa  kwa  watu wenye ulemavu mkoa  wa  Mara  na  kushirikisha  wakuu  wa idara mbalimbali   za  serikali  na sekta binafsi mkoani mara.
 
Amesema  SHIVYAWATA iliwasilisha   kwa iliyokuwa Tume  ya Mabadiliko ya Katiba maoni  mengi  yenye  maslahi  pia  kwa  watu wenye ulemavu  ukiwemo  uwakilishi  katika vyombo  vya  maamuzi, lakini cha  kushangaza  katiba  hiyo pendekezwa imepuuza baadhi   ya  maoni  hayo.