Jumatatu , 27th Jun , 2016

Serikali imesema imeanzisha utaratibu mpya wa kusajili dawa za Waganga wa Tiba Asili na Tiba Mbadala ili kudhibiti watumiaji wa dawa hizo kupewa dawa zisizo na viwango na nyingine kudaiwa kuwa na vimbata vya sumu.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Hamisi Kigwangala

Akizungumza leo Bungeni Mjini Dodoma, katika kipindi cha Maswali na Majibu, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Hamisi Kigwangala amesema utaratibu huo utadhibiti kwa kiasi kikubwa madhara yatokanayo na dawa hizo.

Mhe. Kigwangala pia amewataka waganga wa tiba asili na tiba mbadala ambao hawajasajiliwa wanapaswa kufuata utaratibu wa kisheria uliopo sasa ili watambulike kisheria na huduma wanazozitoa.

Katika hatua nyingine Mhe. Kigwangala amesema serikali kwa sasa imeweka mfumo thabiti ambao unatumiwa kwa ajili za kupitisha dawa kwa ajili ya matumizi ya binadamu na mifugo nchini ili kudhibiti matumizi ya dawa feki.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Khamisi Kigwangala