Jumatatu , 28th Dec , 2015

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia watoto na wazee imesema kuwa bado kuna maambukizi mapya ya ugonjwa wa kipindupindu hapa nchini, na kusisitiza kuwa agizo lake la kupiga marufuku uuzwaji wa matunda pamoja na chakula lipo pale pale.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamiin Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Afya

Akitoa taarifa ya hali ya Ugonjwa wa kipindupindu hapa nchini leo jijini Dar es salaam Waziri Ummi Mwalimu amesema kuwa mpaka leo kuna wagonjwa wapya 76 hapa nchini toka mikoa 21 huku watu 196 wamefariki huku mkoa wa Kigoma ukiongoza kwa kuwa na wagonjwa wapya 17 ikifuatiwa na Morogoro vijijini 12 na Iramba 7 na kwingineko.

Waziri Mwalimu ameongeza kuwa agizo lake la kupiga marufuku uuzwaji wa matunda yaliyokatwa upo pale pale pamoja na Kuuza chakula katika mazingira machafu,

Aidha Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii, jinsia watoto na wazee watoto watakuwa wakitoa taarifa ya ugonjwa wa kipindupindu kila jumatatu pamoja na kuzitaja halmashauri zinazoongoza kwa maambukizi.