Jumatano , 3rd Aug , 2016

Serikali imeombwa kuingilia kati vitendo vya ukatili na udhalilishaji wanavyofanyia baadhi ya wakristo wanaopinga tohara za kimila katika jamii ya kimasai na badala yake kusimamia misingi ya kikatiba kuwa kila mtu anahaki ya kuabudi,

Mchungaji Moses Baraka wa Kijijini Lesiraa

Moses Baraka na Rarael Ezekiel ni wakazi wa kijiji cha Lesiraa Kata ya kisongo ambao wanadaiwa kuvuliwa nguo na kutembezwa yapata vijiji vitatu ikiwa ni sehemu ya adhabu, kufuatia kutahiri watoto wake hospitali jambo linalopingwa na vingozi wa jamii hiyo vitendo ambavyo vinadaiwa kuwa vikifanywa na vijana wa kimasai.

Kufuatia adha hiyo waliyoipata Mchungaji Moses ameiomba serikali kuingilia kati muingilio uliopo hivi sasa kati ya dini na mila ili kuendeleza amani iliyopo hivi sasa kwa iwapo hali hii itaendelea madhara makubwa zaidi yanaweza kutokea.

East Africa Radio, imeongea na moja wa wanafamilia ambao wazazi wake wamekubwa na adhabu hiyo na kueleza athari walizo pata mara baaada ya mzazi wake kudhalilisha .

Hata hivyo viongozi wa kijiji cha Lesira hawakuwa tayari kuzungumzia swala hilo kwa madai kuwa swala hilo limefikishwa katika ngazi husika.

Sauti ya Mchungaji Moses Baraka wa Kijijini Lesiraa