Jumatano , 3rd Feb , 2016

Matokeo ya hati chafu katika baadhi ya halmashauri nchini yanadaiwa kutokana na kutokuwepo kwa ushirikishwaji hususani wa watendaji ambao wengi wao hawatambui wajibu wao katika sheria ya manunuzi ya umma wakati wa utekelezaji wa majukumu yao .

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha Bi. Tatu Selemani

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha Bi. Tatu Selemani amesema hayo mjini Morogoro wakati wa kikao cha watendaji wa halmashauri za wilaya ambapo ameshauri pamoja na kuzingatiwa kwa matumizi sahihi ya manunuzi ya umma ni vyema watendaji kutambua wana uwezo wa kutoa maamuzi sahihi ya manunuzi ya umma na kuzinusuru halmashauri zao ziepukane na kupata hati chafu

Kwa upande wake mratibu wa mafunzo yanayotolewa na serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na shirika la kiteknolojia la ubelgiji(BTC) Abbas Kajwangya amesema, mpangilio wa kutoa elimu kwa watendaji wa halmashauri unatokana na matokeo mabaya katika baadhi ya halmashauri hivyo kupata hati chafu.

Halmashauri 28 za mikoa ya Pwani, Tanga, Dodoma na Kigoma wamenufaika na mafunzo yanayolenga kuwaelimisha watendaji 620 kuhusu uandaaji wa taarifa katika halmashauri, kuandaa mpango wa manunuzi, ulipaji kwa kutumia mitandao na sheria za manunuzi ya umma.