Jumapili , 17th Jan , 2016

Waziri wa Fedha nchini Dkt. Philip Mpango amesema tayari Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imeandikia barua benki ya Stanbic ya kusudio la kuitoza faini ya shilingi bilioni 3, baada kugundua matatizo yaliyohusiana na hasara itokanayo na mikopo katika benk

Waziri wa Fedha nchini Dkt. Philip Mpango

Dkt. Mpango amesema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwa lengo la kutoa taarifa kwa wananchi, kuhusu hatua ambazo zimechukuliwa dhidi ya benki ya Stanbic Tanzania Limited kuhusana na ushiriki wake kuwezesha mkopo wa serikali wa dola za Marekani milioni 600..

Aidha Dkt. Mpango amesema benki kuu imechukua hatua hizo kama onyo kwa benki ya stanbic na ili iweze kuwa makini katika kuhakikisha kuwa shughuli zake zinaendeshwa kwa mujibu wa taratibu za kibenki na kuzingatia sheria.

Dkt. Mpango ameongeza kuwa hatua hiyo ni onyo kwa mabenki na taasisi za fedha zisijihushishe na makosa ya ya aina hiyo ambayo ni kinyume cha taratibu za kibenki na ni uvunjaji wa sheria za nchi.