Jumanne , 11th Aug , 2015

Serikali imesema imejianda kikamilifu kukabiliana na matumizi yote mabaya ya mitandao hasa katika mitandao ya kijamii katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika oktoba 25 ili kuepuka Uchochezi ,vurugu na kuhatarisha Amani.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea na viongozi wa Wakala ya Serikali Mtandao na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Dkt. Ali Simba ambae ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Serikali mtandao toka Ofisi ya rais menejimemi ya utumishi wa Uma katika mkutano uliowakutanisha Wadau wote muhimu wa sekta ya mifumo ya kompyuta na tehama.

Dkt. Simba ameongeza kuwa Kwa jinsi ambavyo teknolojia inavyokuwa kwa kasi duniani ndivyo na makosa na Uhalifu wa mitandaoni inavyoongeza,

Aidha Dkt. Simba amesema kuwa Kupitia sheria mpya ya makosa ya mtandaoni na kushirikiana na Polisi na Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA Wataweza kudhibiti maneno ya Uchochezi na Vitendo vyote vinavyolenga kuharibu Utulivi na Amani iliopo nchini.