Jumamosi , 26th Sep , 2015

Serikali imeombwa kupitia upya mfumo wa biashara ya kuuza pombe, pamoja na kuangalia uwezekano wa kutenga kodi, itokanayo na bidhaa hiyo, ili ihudumie madhara yanayosababishwa na unywaji wa pombe.

Mtafiti na mwanaharakati wa afya ya jamii, Dk. Bertha Maegga

Hayo yameelezwa jana wilayani Arumeru mkoani hapa na Mtafiti na na mwanaharakati wa afya ya jamii, Dk. Bertha Maegga,,kwenye warsha ya washiriki wa ,wanaoshughulika na matatizo yatokanayo na pombe kutoka nchi za Afrika Mashariki(EAC).

Amesema mpaka sasa nchi za EAC, bado zinakabiliwa na changamotio kubwa ya udhaifu katika sheria, udhibiti wa baishara ya pombe.

Dk. Betha amesema zamani kulikuwa na sheria inayodhibiti wakati wa unywaji wa pombe, lakini siku hizi taratibu na biashara ya pombe zimebadilika maduka ya kuuza pombe yanafunguliwa asubuhi, kinyume na sheria.

Amesema sheria yetu ipo nyuma sana, inatakiwa kurekebishwa kwani hivi sasa pombe inauzwa mpaka kwenye maeneo ya makazi.

Dk. Maegga amewaomba watunga sera waangalie maeneo yanayotokana na madhara ya pombe kutokana na kutokuwapo mpango wa kuwasaidia watu wanaopatwa na madhara ya pombe.

Naye mkurugenzi wa mipango na uhamasishaji Maik Dunnbier wa Taasisi ya IOGT, amesema Tanzania kama zilivyo nchi za Afrika Mashariki na mataifa mengine duniani, inakabiliwa na tatizo kubwa la madhara yatokanayo na pombe.