Jumapili , 18th Apr , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amewataka wabunge kuwa na mijadala inayojikita katika kupitisha bajeti za serikali kwa ajili ya maendeleo ya taifa badala mijadala amabayo haina tija kwa taifa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan

Rais Samia amesema hayo katika Kongamano la kidini la taifa liliofanyika Dodoma ambapo ameeleza kuwa awamu ya Sita imeikita kuendeleza na kudumisha mema yaliyopita, yaliyopo na mapya na hiyo  ndio maana halisi ya kauli yakke ya ‘Kazi Iendelee' kwani kazi ilishafanywa hiovyo inaendelezwa .

“Nimekuwa nikifuatilia mijadala yenu bungeni, ni mijadala ambayo haina afya kwa taifa letu naomba sana kipindi hiki ndugu zangu wabunge tunatakiwa kupitisha bajeti za sekta mbalimbali, bajeti ya serikali kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu naomba jikiteni sana huko" amesema  Rais Samia

Pia Rais Samia ameeleza kuwa tiyari ameshaunda kamati ya kumshauri kuhusiana na hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa kama nchi kuhusuiana na anga la virusi vya corona.

“Nataka niwape taarifa kwamba tayari nimeshaunda kamati ya kunishauri kuhusu hatua tunazoweza kuchukua kama nchi jinsi tutakavyojikinga na janga la corona, na hivi punde nitakaa nao na uongozi wa Wizara ya Afya na Wizara ya Fedha ili kuona namna tutakavyokwenda na jambo hili” amesema Rais Samia