Jumanne , 19th Jul , 2016

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana, ametoa onyo kwa watu wote wanaotaka kufanya fujo kwenye mkutano mkuu maalum wa CCM kuwa Dodoma siyo mahali salama kwao.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana

Mkutano mkuu maalum wa CCM, unatarajiwa kufanyika mjini Dodoma Julai 23 mwaka huu ambapo Mwenyekiti wa CCM Dk Jakaya Kikwete anatarajia kuamwachia nafasi hiyo Rais John Magufuli huku kukiwa na tishio la baadhi ya vijana kutoka vyama vya upinzani kuuzuia mkutano huo.

Rugimbana amesema mkutano huo wa CCM unafanyika kwa mujibu wa sheria na taratibu za chama hicho hivyo hakuna mtu yeyote anayetaka kuvuruga mkutano huo atakayevumiliwa.

Aidha amewatoa hofu wananchi wa mkoa wa Dodoma na wageni wote watakaokuja kwenye mkutano huo kuwa hali ya ulinzi na usalama katika kipindi chote cha mkutano huo umeimarishwa.