Ripoti ya waliozaliwa Januari 1, 2021 Muhimbili

Ijumaa , 1st Jan , 2021

Katika usiku wa kuamkia mwaka mpya, Januari 1, 2021, jumla ya watoto 6 wamezaliwa katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili - Upanga.

Picha ya Muhimbili

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na idara ya Habari ya Hospitali hiyo, kati ya watoto hao wanne ni wakiume na wawili ni wa kike.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa watoto wanne wamezaliwa kwa njia ya kawaida na wawili kwa njia ya upasuaji. 

Kuhusu afya zao, taarifa imeeleza kuwa watoto wote wapo salama pamoja na mama zao wote wana afya njema kabisa.