Jumatatu , 17th Nov , 2014

Hatimaye Naibu Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai amekabidhi rasmi taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG inayo husu wizi wa zaidi ya shilingi Bilioni 200 fedha zilizokuwa katika akaunti ESCROW.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Job Ndugai akikabidhi Ripoti maalumu ya CAG Kuhusu akaunti ya ESCROW kwa Mwenyekiti wa PAC Mhe. Zitto Kabwe na Kaimu wake Mh. Deo Filikunjombe,Bungeni mjini Dodoma leo

Hatimaye Naibu Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai amekabidhi rasmi taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG inayo husu wizi wa zaidi ya shilingi Bilioni 200 fedha zilizokuwa katika akaunti ESCROW kwa kamati ya kudumu ya bunge ya hesabau za serikali PAC.

Akikabidhi taarifa hiyo, Naibu Spika Mh. Job Ndugai ameitaka kamati ya PAC kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni ya Tatu na Nne ya nyongeza ya saba ya kanuni za kudumu za bunge za mwaka 2014 na kifungu cha tisa na kifungu 31 ya sheria ya haki, kinga na Madaraka ya Bunge.

Akizungumza na waandishi wa habari, mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya hesabu za serikali Mhe. Zitto Kabwe amepongeza hatua ya Naibu Spika kukabidhi taarifa hiyo na kuahidi kamati yake itafanyakazi kwa kuzingatia kanuni ikiwemo kufanya uchunguzi.

Wakati huohuo katika mkutano wa 16 na 17 wa Bunge, baadhi ya wabunge wameomba mwongozo wa Spika kutokana na madai ya baadhi ya mawaziri kutoa majibu mepesi, huku wengine wakiendelea kusisitiza mawaziri mizigo kuondolewa katika wizara husika kutokana na kusaidia kuondoa kero za wananchi hususani wakulima wa pamba.

Katika hatua nginyine waziri mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda amesema serikali imetoa kauli kuhusu mauaji ya watu kumi wakiwemo wakulima na wafugaji yaliyotokea Kiteto na kulitaka jeshi la polisi kuwakamata watu wote walioshiriki katika mauaji hayo.