Mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongela
Viongozi hao ni mbunge wa zamani wa jimbo la Ngorongoro Kaika Ole Telele, Diwani wa kata ya Eyasi, Augustino Lukumay, Diwani wa viti maalum wa Kata ya Eyasi Veronica Litiga pamoja na kiongozi wa kabila la Wadatoga.
RC Mongella amesema kuwa tathmini ya muendelezo wa awamu ya tatu ya wananchi waliokubali kuhama katika eneo hilo na kwamba kundi hilo lenye kaya 25 litaanza safari Alhamisi ya wiki hii.
Mongella amesema hatua hiyo inaleta matumaini makubwa katika mchakato huo na kubainisha kuwa viongozi hao kwa pamoja wamekiri kuwa wapo tayari kuhama kwa hiari kwenda Kijiji cha Msomera kwa lengo la kupisha shughuli za uhifadhi.