Alhamisi , 18th Aug , 2022

Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza umuhimu wa usalama wa chakula katika ukanda mzima wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) na kuzisihi nchi hizo kuwekeza kwenye uchumi buluu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Rais Samia amependekeza hayo katika mkutano wa 42 wa SADC uliofanyika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Akizungumzia uwiano wa kijinsia waliokubaliana katika unanda huo, Rais Samia amesema Tanzania imejitahidi kutoa fursa kwa wanawake hasa katika nafasi za uongozi wa kimkakati.

Miongoni mwa nafasi za hizo ni uongozi serikalini na bungeni na zile za uwaziri wa ulinzi, mambo ya nje, uwekezaji, utalii pamoja na nafasi ya Spika wa Bunge.

Rais Samia alitoa maoni yake kwa lugha ya Kiswahili ikiwa ni jitihada za kuchapusha matumizi ya lugha hiyo miongoni mwa nchi za SADC.

Katika mkutano hupo uliopitisha maazimio 27 , Rais Samia amesistiza uharakishwji wa mchakato wa Kiswahili kupitishwa rasmi kama lugha ya nne ya jumuiya ya SADC.

Mkutano huo wa SADC pia ulishuhudia makabidhiano ya uenyekiti kutoka kwa Rais wa Malawi Dkt Lazarus Chikwera na sasa nafasi hiyo ikichukuliwa na Rais Felix Tshisekedi  wa DRC.
Rais Samia anatarajiwa kufanya ziara ya siku moja nchini DRC hii leo na atafanya  mazungumzo na mwenyeji wake Rais Felix Tshisekedi.