Rais Magufuli ataraji kumpokea Rais wa Msumbiji

Jumapili , 10th Jan , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kesho Januari 11, 2021 anatarajia kumpokea Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Filipe Nyusi katika Uwanja wa Ndege wa Geita uliopo Chato.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli akiwa na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Filipe Nyusi.

Akitoa taarifa hiyo kwa wanahabari Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuwa ziara hiyo itakuwa ya siku mbili ambayo itakuwa ya kizazi na kuendelea kuimarisha mahusiano baina ya Tanzania na Msumbiji.

Ziara hii ilitakiwa kufanyika Oktoba mwaka jana lakini kutokana na sababu zilizoshindwa kuzuilika haikufanyika, hivyo Rais Filipe atawasili kesho”, amesema Prof. Kabudi.

Akizungumzia uhusiano uliopo baina ya Tanzania na Msumbiji Prof. Kabudi amesema kuwa Nchi hizo wawekezaji wake kutoka pande zote wanafanya biashara kwa mwenzake bila vikwazo na mafanikio makubwa.